KILELE CHA UBEPARI TANZANIA NA AFRIKA
Afrika imefika hapa
ilipofika sasa kwa sababu wazee wetu waliviona hivi viashiria vya ubepari toka
mwanzo lakini hawakuchukuwa hatua za msingi kuvidhibiti zaidi ya wengi wa wazee
wetu walizidi kukuza fadhila za walowezi wakiamini ndio mwazo wa maendeleo
katika nchi zetu.Elimu ya kugundua kuwa hivi ni viashiria vya ubepari katika
afrika na vina madhara gani kwa usitawi wa bara letu ilikuwa bado ndogo ndani
ya viongozi wetu na wananchi kwa ujumla.
Shukurani za dhati kwa
HAYATI MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE kwa kuona hili mapema na kugundua kuwa
makabila na dini ni zao la ubepari hivyo basi akaunda serikali isiyoegemea
kwenye kabila lolote au dini yoyote ile. Akasimamia umoja wa kitaifa ingawa
ilikuwa ngumu sana maana machifu na wakuu wa koo walikuwa wameshalewa na
ubepari huu mdogo ndani ya roho zao.
Mwalimu akishirikiana
na waasisi wengine wa taifa wakatengeneza azimio la Arusha lengo lilikuwa moja
tu kujaribu na kuhakikisha huu ubepari mdogo unaisha ndani ya nchi.Wakasimamia
kwa nguvu zao zote lakini kazi ikawa bado ngumu.
Azimo la Arusha
liliposhinda kufanikiwa nchini ilikuwa ni sherehe tosha kwa mabepari wa dunia
hii maana lingeleta kikwazo kikubwa kwao katika utekelezaji wa shughuli zao za
kila siku nchini kama wananchi wote wangelikubali kwa roho moja.
Hili ndilo lilikuwa
pigo kubwa kwa masikini wote wa taifa hili, pindi mkombozi wetu(azimio la
Arusha) alipofariki baada ya kushindwa nguvu na mabepari neema yetu,asali
yetu,saruji yetu,chakula chetu,na kila kitu chetu kilikufa nae.
Azimio liliondoka na
faraja ya masikini Tanzania, faraja ya
masikini afrika ,faraja ya masikini wa dunia.Mizani ya usawa ikavunjika vipande
vipande kutokana nakuelemewa na mzigo wa upande mmoja.
Mimi alipata nguvu
kubwa kuliko sisi.wachache wakawa wakuu wa maamuzi kuliko wengi, wazawa wakawa
wageni barani afrika na wageni wakawa wazawa.huu ndo ufalume wa ubepari ulipo
fanikiwa na kutupa walo wengi chini hi indo maana ya kura ya VETO.
Mtu mmoja ana uwezo wa
kutumia kura yake kupinga kura za taifa zima au jumuiya zima hivyo wangonge
wanakuwa hawana tena dhamani mbele ya wachache wanaoweza kupiga kura juu ya
mstakabali wa maisha yao ya sasa na baadae.
Elimu inamchango mkubwa
wa waziwazi wakuuwa usawa(ujamaa) katika nchi nyingi za afrika.Tukiangalia
elimu ya kikoloni ilimjenga mtu kuwa tofauti na wengine kuwa na aina tofauti ya
jamii alipotokea.mbinu nyingi za uzalishaji na utunzaji kumbukumbu kitu ambacho
kiliwafanya wengi wazitumie mbinu hizo vibaya kwa kuiba na kudhulumu kirahisi.
Elimu ilimfanya mtu
kujisikia, kupenda anasa na maisha ya kifahari kitu ambacho kilichangia kwa
kiasi kikubwa kuuwa ujamaa uliokuwa nchini.tukumbuke kuwa Mwalimu Julius
kambarage Nyerere alijitahidi kwa kiasi kikubwa kuondoa hali hii ndani ya nchi
yetu lakini alishindwa kutokana kukosa ushirikiano ndani ya wasomi wa nchi hii
walikuwa wanataka kazi nzuri nyumba zuri na maisha ya kifahari kuliko hata hali
halisi ya taifa letu.
Mila na desturi zetu
zilizowafanya machifu kuwa na mali nyingi na wake wengi kwa kiasi Fulani
zilipunguza mvuto wa ujamaa na kujitegemea maana chifu alikuwa na wingi wa mali
kuzidi jamii iliyomzunguka hali hii kwa kiasi Fulani ilileta chuki ndani ya
jamii.
Sababu nyingine nyingi
kama ongezeko la watu, ugumu wa ufatiliaji,ukubwa wa nchi,na majanga ya kitaifa
kama vile njaa viliweza kupunguza kasi ya azimio la Arusha kwa kiasi fulani.