SK FOUNDATION
SK Foundation ni shirika lisilo la kiserekali,lliloanzishwa
rasmi tarehe 2/8/2013 na ndugu Frank
.A.Lyimo.SK Foundation ikibeba maana ya “SOMA KITABU FOUNDATION ”.Sababu kuu
iliyo mfanya mmiliki wa SK
NETWORK,VIPEPERUSHI COMPANY NA HOME OF FIGURES
ndugu FRANK .A. LYIMO kuanzisha hii foundation ni kutokana na kundi
kubwa la vijana wa kiafrika kutopendelea kusoma vitabu kabisa.Hali hii imefanya bara letu kuwa nyuma
kimaendeleo na kushindwa kukabili changamoto
mbali mbali za kisiasa na kijamii kutokana na uelewa mdogo wa mambo
yanavyokwenda dunia.Ili kuweza kurudisha kuiokoa Afrika na hili janga la
ukosefu wa maarifa ni jukumu letu sote kuhamasishana kusoma vitabu kwa wingi ili
kupata maarifa mpya kila wakati.Kutokana
na vijana ndio nguvu kazi kubwa ya
taifa,ndio maana aliamua kuwahamasisha
vijana kusoma vitabu kwa nguvu zote ili waweze kupata maarifa na waweze
kuyatumia kujenga taifa letu la Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Dhumuni la SK foundation
Dhumuni kuu la sk foundation ni kuhamasisha vijana wa
Tanzania na waafrika kwa ujumla kusoma vitabu kila wakati kwa maendeleo yao na
taifa kwa ujumla.
Kauli mbio yetu
Soma kitabu ongeza maarifa.
MAWASILIANO
Tupo ubungo msewe
Dar es salaam
Fax +255 736604852
Simu namba:+ 255 767 592224
+255 713 592224
Barua pepe: somakitabufoundation@gmail.com
Tovuti: www.somakitabu.blogspot.com
Kazi zetu
Kuhamasisha vijana kujenga tabia ya kusoma vitabu kupitia mitandao ya kijamii na vipeperushi.
Kukusanya vitabu vinavyofaa kusomwa na vijana na kuvisambaza
kwa vijana wote Tanzania na afrika
Kukutana na watunzi wa vitabu kwa mwaka mara mbili ili
kuratibu sindano la usomaji vitabu
Kuihimiza serekali kusambaza vitabu kwa wingi kwenye
maktaba,mashule na vyuo ili vijana wapate kuvisoma kwa urahisi
Kuhimiza serekali na wadau wengine kujenga maktaba za kisasa
kila kona ya nchi ili vijana wapate sehemu bora na tulivu za kujisomea.
Kujiunga nasi
Unaweza kujiunga
nasi na
tukafanya kazi pamoja ya kuhamasisha vijana kusoma vitabu kwa manufaa
yao na ya taifa kwa ujumla.Tutumie barua
pepe yenye maelezo yote muhimu na
dhumuni la kutaka kujiunga nasi.
Kuchangia
Unaweza kuchagia mawazo,fedha au chochote kile unachoona
kinafaa na kitasaidia kukuza na kuendeleza
shirika hili ili liweze kuwafikia vijana wengi na kutoa huduma kwa
ufanisi zaidi.
“ soma vitabu ongeza maarifa,okoa taifa”
No comments:
Post a Comment