Wapi tumekosea?
Tulipokosea ni pale
tulipo kubali kuishi na kukumbatia katiba isiyo na manufaa kwetu na kwa kizazi
chetu cha sasa na baadae. Wengi wetu tulikuwa hatujui ni kipi hasa wanakifanya
wanasiasa wa nchini zetu na nguvu yao ni
ipi na inawezaji kuathiri uhai wa nchi yetu kama hawatotumia hekima yao katika
kutoa maamuzi makini?(tuliiacha siasa ijiendeshe yenyewe)
Tulifanya vingi kwa
mkupuo mmoja na kusahau dhumuni letu la awali na tabia hii tunaendelea nayo
hadi sasa(tunakusahiki tunaacha tuagusa kingine kabla cha mwazo hakijaisha)
Kuiga mambo ya ulaya
kumetupoza kwa kuwa wale tunaowainga miaka hamsini nyuma walitunyonga na
kutuchapa mijeledi sasa badala ya kudai fedia na kuwawekea sheria kali viongozi
wetu wakawanaenda kuomba maji mtoni wakati kwao wameacha bahari.hii ndo faida
ya kujidharau mwenyewe..Tulijidharau na tukaangaika kutafuta wenye akili ili
hali tulikuwa na akili nyingi kuzidi wao.
Wasaliti Afrika wenzetu
waliamua kwa dhati yao kuuza taifa kwa mikataba mibovu huku wakisisitiza usiri
katika mikataba yetu, maana usiri ni mama wa ubinafsi na ubinafsi ni motto wa
ubepari.
Kukumbatia elimu yao isiyo na manufaa inapoteza muda
mrefu na inazalisha wategemezi wengi (kizazi cha starehe na fasbuku)kuliko
wabunifu ambao ndo tunawahitaji kwa sasa.kwa ujinga wetu tukaacha kuchukua
hatua za dhati kukuza sayansi kama China.Tukachakachua elimu yetu wenyewe na
siasa huku tukitegemea tutakuwa kiuchumi kwa kuwa na vyuo vya kozi maneno.. yakatoka Malipo ya ujinga wetu sasa
nchi zetu zinawanasiasa wengi kuliko na kila mtu ana tai na suti tunapishana
posta tukitafuta ajira.je hapa taifa litakuwa kweli?
Wanyoge kukosa umoja,
wengi wa watu wa hali ya chini hatuna umoja
katika kutetea masilahi yetu na taifa kwa ujumla.Hii inatokana na tishio
tunavyopata kwa wale la tunaodai na
hutumia njia mbaya za kututenga tusifanikiwe?