Je
utasibitishaje hili?
Angalia katika katiba
nyingi za nchi za afrika rasilimali kuu ambayo ni ardhi imeweka chini ya serikali
na rais akawa na mamlaka ya juu ya kutengua matumizi ya ardhi wakati wowote.Hii
ilifanya kazi rahisi kwa walowezi(wezi) wakarudi bila shida na tukawapokea kwa
shangwe na nderemo bila vipingamizi wakiwa ndo wale wale wajukuu na watoto wa
wale waliotutesa miaka 20 nyuma,tukaambiwa eneo hili watafanyia uwekezaji na
tutapata ajira hivyo tuliwaachia maeneo yetu ya mila na desturi maeneo ya
matambiko wakajenga majumba na sisi tukaamia kilimani eneo lenye mawe mengi na
ndorobo.Je ni nini kilichotufanya tuwaamini kuwa hawa sasa ni marafiki wetu wa
dhati si maadui kama awali ilivyokuwa wakituchapa mjeledi na kutusulubisha?je
ni uhuru ndo ulituunganisha kwa haraka?jibu hapa ni ndio uhuru ulitupumbaza
sana waafrika na kuaamini hawawezi tena kutuzidi akili kama awali.hivyo hata
kama walija watakuja na sisi indo wenye nchi watakuwa wanatuogopa na hawato
tuonea tena.hizi ndo zilikuwa hisia nyingi za wanyonge wakiamini kitu wasijicho
kijua kiundani.