Uwekezaji
afrika ulitokea wapi?
Uwekezaji ulizaliwa
baada ya kuwepo na uzalishaji mkubwa wa bidhaa barani ulaya na amerika ya
kasikazini. Wingi wa viwanda ulihitaji sana malighafi za kutosha ili
kufanikisha uzalishaji, hivyo basi wakaamua kuja afrika na kuwekeza katika
viwanda vya kutafuta malighafi.
Ongezeko la masoko
lilifanya mabepari wafikirie upya na kuamua kuanzisha viwanda vidogo vidogo
barani afrika ili kuteka soko lililokuwa linachipukia.
Kwa kuwa Afrika ilikuwa
eneo lilikuwa na rasilimali za kutosha na kukufanya kazi ya uvunaji wa
rasilimali ifanye usiku na mchana huku wakilindwa na sheria za nchi zetu ambazo
kwa asilimia kubwa wanamchango wao hapo katika kuzitunga na hivyo basi wanajua
ni jinsi gani wacheze nazo pindi tatizo linapotokea?ingawa katika nchi kadhaa
za afrika waliweza kufukuzwa pindi tu nchi hizo zilivyopata uhuru lakini
hawakukawia kurudi baada ya kitambi kidogo kupita.Wakaja na stimuu mpya ya
kungata na kupuliza unayotumika mpaka sasa na viongozi wengi wa afrika na ulaya
kwa ujumla.