Toka enzi tunaona kuwa
babu zetu na bibi walibebesha pembe za ndovu na dhahabu zao wenyewe huku fimbo
zikimiminika migongoni mwao na wengine kubakwa wakiwa njiani na mbaya zaidi
hali hii ilifanya watu hawa kuwa watumwa ndani ya maeneo yao wenyewe. Waliokufa
hakuna aliyejitokeza kuwazika, wakalia lakini hawakufutwa machozi, wakazaa huku
wakiwa napingu vichwani mwao huu ndio ulikuwa ukaribisho rasmi wa ubepari kwa
afrika hiki ndicho kiashiria cha ukosefu wa utu pindi watu Fulani watakapoamua
kuisaminisha mali ikawa na dhamani kuzidi utu wa mtu.hapa ndipo ilizaliwa lile
neno lisemalo bora punda afe mzigo ufike.je punda alikuwa nani?punda ndio sisi
waafrika tuliokufa tukiwa na mnyororo shingoni ili tu pembe za ndovu zifike
pwani.