Katika hali ya kawaida
tunaona kuwa dhumuni kubwa la ubepari dunia
ni uuwaji,nikimaanisha kuwa shetani alikuwa anaamini kuwa pindi adamu na
eva watapomsaliti mungu basi mungu atawaacha wapweke na kwa sababu ya mateso na
masumbuko ya dunia watu hawa watashindwa kusitahimili mateso hayo na kufa na
kuacha mali zote chini ya hima yake muovu shetani.
Imani ya shetani
ilikuwa kuu akiamini kuwa hata kama wataweza kuzaa na kuongezeka basi kizazi
watachokizaa watakirisisha dhambi kuu ya ubinafsi ambayo ni kitovu cha ubepari na
mwisho wa nyakati watauana wenyewe kwa wenyewe wakigombania malisho na chakula.