Tujikumbushe kwanza
Africa ilitoka wapi ?Africa kama mabara mengine dunia lilikuwa bara lenye wananchi wanaojiongoza
kwa mila na desturi za makabila yao.Hii
ikimaanisha kuwa sheria na taaratibu za kuishi zilizingatia sana mila na
desturi hiyo basi kila ukoo ulifanya kila mbinu ili uweze kukubalika katika
kabila husika na waweze kupewa uongozi wa kabila husika,hali hii ilifanya kupatikana
kwa ukoo zenye nguvu ya kutawala na kutoa maamuzi mazito kuhusu makabila
husika.
Katika hali hii iliongeza ubunifu hasa katika
maeneo ya uzalishaji wa mazao na vifaa vya kivita na mafunzo ya kijeshi.hii
ilisaidia sana ukuwaji wa maeneo na kusababisha koo na makabila mengine madogo
madogo kufa kwa sababu ya kushindwa
kivita na mali zao walizokuwa wakimiliki kupokonywa na makabila hayo
yakageuka vibaraka wa makabila yale makubwa.
Makabila mengi
yalipotea nakutofahamika tena kwenye uso wa dunia kutokana na sababu hizo na
mengine yaliweka makazi kwenye maeneo yenye wanyama wakali ,mafuriko na wadudu
waambukizao maradhi na wakashambuliwa na
magonjwa,wanyama wakali na mafuriko na
kuisha taratibu baada ya kuanza kutawanyika kukimbia majanga hayo.