Faida ya ujamaa ilikuwa
ni ipi kwa Tanzania?
Ujamaa na kujitegemea
hili ndilo kusudio la mungu kwa watu wake, waishi kwa umoja na ushirikiano
ndani ya hii dunia.kila mmoja amsaidie wenzake na kuwepo na usawa baina ya mtu
na mtu.
Kwa kiasi kikubwa
tuliweza kufanya mengi ya kujivuna pindi tulipokuwa tumeshikamana tulijenga
reli,barabara,bandari,hospitali,shule na vingine vingi ambayo vimeshindwa hata kuendelezwa
na viongozi wa sasa na kuviacha vife kwa kukosa usimamizi.hapa nipo utengano
unapoonyesha wazi kuwa hauwezi kutukomboa wanyonge tunaotegemea reli ambayo
inachechemia sasa na kufanya wenye nacho kutubeba kwa magari yanayotupa shida
kila siku huko barabarani.umoja ni nguvu toka umbaji na anayekataa umoja ni
mwenye dhambi na ardhi yake hulaaniwa na Mungu hiki ndicho kimetukuta sasa
tunashindwa kwenda mbele tunashindwa kurudi nyuma.