Nini tufanye?
Kwa haraka cha kufanya
ni kuunda umoja na kudai mabadiliko ya dhati.
Kufufua azimio la
arusha kwa nguvu zote.
Kufilisi wale wote
waliotuibia rasilimali zetu na kuwafunga jela.
Kuunda mikataba mipya
kwa wawekezaji wote nchi.
Je utajiuliza tutawezaje
vyote hivi jibu ni rahisi tu, Umoja ni nguvu tukiwa wamoja tutaunda taifa jipya
na lenye mavuno bora zaidi(katiba mpya)
Afrika
Katika kipindi chote
hiki tunapo shuhudia mabadiliko makubwa katika bara la afrika ni kwa sababu ya
kuchoka kwa wananchi ugandamizwaji unaofanywa na walowezi na waafrika wenzetu
wasio na nia njema wanakula keki ya taifa wachache na kutuacha maelfu tukifa
kwa utapiamlo.
Makundi ya wanyonge
walalamika na kudai mabadiliko ya dhati kutoka kwa viongozi wao lakini yalishindikana
kwa kuwa ubinafsi hujengwa na roho na ni ngumu sana kubadilisha roho ya mtu.
Ardhi ya babu na bibi
yangu Africa ilishuhudia damu ikimwagika mnyonge akipigwa bom na ili afe.ubinafsi
huondoa uti ubepari haudhani roho ya myonge.
Mabepari wakauwa ndugu
zetu wakawachimbia chini na kuwazika.lakini wachache waliobaki walipata nguvu
pindi walipokuwa wanaenda mazishini kuzika wenzao na wakaamua wafie nchi kwao.
Mungu
awalaze mahala pema peponi wanyonge wote waliofia mataifa yao wakipinga ubepari.